1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE: Kodi yapandishwa katika bidhaa kadhaa

18 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEk8

Serikali ya Zimbabwe imepandisha kodi ya bidhaa kadhaa ili kuziba pengo linalotokana na matumizi makubwa katika kukabili athari za ukame na kampeni ya kuyavunja makaazi ya walalahoi.

Waziri wa fedha bwana Herbert Murerwa amesema kwamba kodi itaongezeka kwa asilimia 50 katika vinywaji na sigara.

Kodi pia itapandishwa kwa asilimia 22.5 katika matumizi ya simu za mkono.

Zimbabwe inakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula,mafuta na fedha za kigeni.Nchi hiyo pia inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira na ongezeko la bei.

Chama cha upinzani nchini humo MDC, kimesema kwamba ongezeko hilo la kodi litasababisha shida zaidi kwa wananchi.

.