1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harare: Kiwiliwili cha rais wa kwanza wa Zimbabwe

13 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CEDr
Kiwiliwili cha rais wa kwanza wa Zimbabwe, Canaan Banana, aliyefariki mjini London mwanzoni mwa wiki hii, kitarejeshwa nyumbani wiki hii, gazeti liliripoti hii leo. Gazeti la serikali Herald lilisema mwili wa Banana utawasili kwa ndege hiyo kesho. Banana, aliyekuwa na wadhifa wa heshima tu kama rais baina ya mwaka 1980 na 1987, alifariki katika hospitali mjini London siku ya jumatatu. Ripoti zinasema alikuwa akiugua kensa. Kasisi wa zamani Banana alirithiwa na waziri mkuu Robert Mugabe mwaka 1987 baada ya kubadilishwa katiba ili kupatia rais mpya madaraka makubwa ya kiutawala.