HARARE: Imani ya kibiashara yazidi kutoweka Zimbabwe
10 Mei 2005Matangazo
Imani ya kibiashara nchini Zimbabwe imezidi kupunguka,baada ya jitahada za serikali kutaka kuchangamsha uchumi uliodhoofika,kuzusha wimbi jipya la upungufu wa chakula,mafuta ya petroli na sarafu za kigeni,wanasema wadadisi.Mshauri maarufu wa uchumi wa kibinafsi,John Robertson amesema ni vigumu sana kuwa na mtazamo wa matumainio mazuri wakati ambapo hali yaonekana kuwa ni ya kukatisha tamaa na wakuu wenye dhima wanatumia takriban wakati wao wote kuwalaumu wengine.