1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE: Hatima ya Zimbabwe na madeni yake

4 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEee

Tume ya Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF haikudokeza cho chote kuhusu hatima ya Zimbabwe,ilipoondoka nchi hiyo iliyokumbwa na matatizo ya kifedha.Zimbabwe wiki hii ilijikusanyia Dola milioni 120 katika juhudi ya kuzuia kufukuzwa kutoka IMF.Tume ya IMF iliwasili Zimbabwe wiki mbili za nyuma,huku Shirika hilo likijitayarisha kwa mkutano wa bodi yake hapo Septemba 9.Mkutano huo utajadili suala la kuifukuza Zimbabwe kwa sababu ya madeni ambayo bado hayakulipwa ikiwa ni jumla ya Dola milioni 295.