Harare: Hakimu wa Zimbabwe akataa rufaa
13 Novemba 2003Matangazo
Hakimu wa Zimbabwe leo amekataa rufaa ya wakurugenzi wa gazeti la kila siku la kibinafsi, akisema gazeti hilo halingestahili kuchapishwa kabla ya kujipatia leseni chini ya sheria mpya za vyombo vya habari. Hakimu wa Harare, Mishrod Guvamombe aliamuru kwamba wakurugenzi wanne wa Jumuia ya Waandishi Magazeti nchini Zimbabwe (ANZ), inayochapisha Daily News wafikishwe mahakamani tarehe 6 Februari mwakani kusikilizwa kesi yao. Kesi dhidi ya gazeti la Daily News -- Gazeti huru la karibuni kabisa nchini Zimbabwe -- imemulika sheria mpya za vyombo vya habari, ambazo wahakiki wanasema zmedhamiria kuwanyamazisha wapinzani wa Mugabe.