HARARE: Chama cha Mugabe kimeshinda uchaguzi
2 Aprili 2005Matangazo
Chama cha ZANU-PF cha rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kimejinyakulia ushindi mkubwa wa theluthi mbili katika chaguzi za bunge zilizofanywa siku ya Alkhamis.Uwingi huo mkubwa bungeni unakipa chama tawala mamlaka ya kuibadilisha katiba.Kura zilizohesabiwa zinaonyesha kuwa chama cha ZANU-PF kimeshinda viti 71 kati ya 120 vilivyogombewa.Na Mugabe ana haki ya kuwachagua moja kwa moja wabunge 30 kutoka jumla ya wajumbe 150 bungeni.Kiongozi wa chama cha upinzani cha MDC,bwana Morgan Tsvangirai amemtuhumu Mugabe kuwa amefanya udanganyifu wa kura ili apate kubakia madarakani.Uchaguzi huu umekosolewa vikali pia na Ujerumani,Umoja wa Ulaya na Marekani.