1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE :Balozi wa Marekani ashikwa na jeshi la Zimbabwe

14 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CES7

Wanajeshi wa Zimbabwe walimshikilia balozi wa Marekani aliyeko Harare wiki hii kwa kuingia katika eneo lililopigwa marufuku kupita watu karibu na makao rasmi ya Rais Robert Mugabe.

Msemaji wa rais George Charamba amesema balozi huyo Christopher Dell anapaswa ajione kuwa ana bahati kuwa hai kwa sababu angeliweza kupigwa risasi na kuuwawa.Akizungumza na gazeti la serikali la Herald amesema balozi huyo ajihesabu kuwa na bahati sana kutokana na jeshi la taifa la Zimbabwe lililomshughulikia hapo Jumatatu lilikuwa ni mahiri.

Wizara ya mambo ya nje ya Zimbabwe ilimshutumu Dell kwa kuingia kwa makusudi katika eneo hilo ili kuzusha mzozo wa kidiplomasia usiohitajika.

Katika baruwa ya kulalamika kwa serikali ya Marekani wizara ya mambo ya nje ya Zimbabwe imeshutumu vikali kitendo hicho cha Dell ambacho imesema ni cha kudharau sheria za usalama za Zimbabwe hali ambayo katu isingeliweza kuvumiliwa katika nchi yake mwenyewe.