1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HANOI:Mazungumzo kati ya Japan na Korea Kaskazini yavunjika ghafla

8 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCL9

Mazungumzo ya kurejesha uhusiano kati ya Japan na Korea Kaskazini, yamevunjika. Mapema bila ya kufikiwa kwa makubaliano yoyote.

Mazungumzo yaliyofanyika katika mji mkuu wa Vietnam Hanoi, hayakuchukua zaidi ya saa moja kabla ya kuvunjika huku kukiwa hakuna tarehe yoyote iliyopangwa kwa mazungumzo mengine.

Maafisa wa pande zote mbili wamekuwa wakilaumina kwa kushindwa kukubaliana katika masuala muhimu..

Hii ni mara ya pili mazungumzo hayo kuvunjika ambapo hapo siku ya jumatato mazungumzo hayo yalivunjika ghafla.