1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamilton apata ushindi wa 93 katika Formula One

2 Novemba 2020

Katika mashindano ya magari ya Fomula One maarufu kama Langalanga Lewis Hamilton aliiendeleza rekodi yake ya ushindi kwa kufikisha 93 katika mashindano ya Emilia Romagna Grand Prix nchini Italia.

https://p.dw.com/p/3km2k
Formel 1 Emilia Romagna Grand Prix | Lewis Hamilton und Daniel Ricciardo
Picha: Getty Images

Na katika mashindano ya magari ya Fomula One maarufu kama Langalanga Lewis Hamilton aliiendeleza rekodi yake ya ushindi kwa kufikisha 93 katika mashindano ya Emilia Romagna Grand Prix nchini Italia jana. Timu yake ya Mercedes ilishinda taji la saba mfululizo la Formula One la wajenzi bora baada ya Hamilton kuongoza mbio hizo huku dereva mwenza Valteri Bottas akimaliza wa pili. Muastralia Daniel Ricciardo wa timu ya Renault alimaliza katika nafasi ya tatu.

Hamilton huenda sasa akamfikia nguli wa kampuni ya Ferrari Michael Schumacher kwa kubeba mataji saba ya ulimwengu, katika wiki mbili zijazo kwenye mashindano ya Turkish Grand Prix.

Reuters, AFP, AP, DPA