Hamburg.Waandamana kupinga Manazi.
15 Oktoba 2006Kiasi cha watu 2,000 walijikusanya katika mji wa kaskazini wa bandari nchini Ujerumani wa Hamburg jana katika kumbukumbu dhidi ya maandamano ya waungaji mkono 180 wa chama cha mrengo wa kulia chenye msimamo mkali cha National Democratic Party.
Watu kadha wamekamatwa wakati waandamanaji wanaopinga Manazi walipopambana na polisi.
Wakati huo huo mjini Nuremberg kusini mwa Ujerumani, watu 2,000 wanaopinga ufashist walifanya maandamano wakipinga maandamano yaliyofanywa na Wanazi mamboleo, yaliyoitishwa kama kumbukumbu ya mwaka wa 60 wa mahakama iliyowahukumu wanachama wa chama cha NAZI cha Ujerumani waliohukumiwa kwa kufanya uhalifu wa kivita mjini humo.
Polisi wamesema kuwa maandamano hayo yalikuwa ya amani.