Hamburg , Ujerumani. Polisi wagundua miale katika maeneo mawili mjini Hamburg.
10 Desemba 2006Polisi wa Ujerumani wamesema kuwa wamegundua ishara katika maeneo mawili nje na ndani ya mji wa Hamburg yanayohusishwa na jasusi wa zamani wa Urusi Alexander Litvinenko , ambaye amefariki mwezi uliopita kutoka na sumu la miale.
Usiku , polisi waligundua kiasi fulani cha miale katika nyumba moja ambayo inamilikiwa na mfanyabiashara wa Urusi Dmitry Kovtun, ambaye alikutana na Litvinenko mjini London kabla ya kufariki.
Siku ya Jumamosi, polisi wamesema wamegundua kiasi kingine cha miale katika nyumba nyingine nje kidogo ya mji huo wa bandari. Kovtun , mmoja kati ya raia wawili wa Urusi ambao walikutana na Litvinenko katika hoteli ya Millennium mjini London Novemba mosi, anasemekana kuwa anapatiwa matibabu mjini Moscow kutokana na miale hiyo ya sumu.