1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAMBURG: Ujerumani 2 Slovakia 1

7 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuL

Ujerumani jana usiku mjini Hamburg iliipa Slovakia kipigo cha mabao mawili kwa moja kwenye mechi ya kuwania kufuzu kwa fainali za mashindano ya ubingwa wa Ulaya mwaka ujao.

Bao la ushindi la Ujerumani lilitiwa wavuni na Thomas Hitzlsperger dakika mbili kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Ujerumani ndio waliotangulia kuliona lango la Slovakia baada ya Jan Duran wa Slovakia kuingiwa na mchecheto na kujifunga mwenyewe.

Ujerumani sasa inaongoza kundi la D kwa pointi kumi na tisa.

Kwengineko Uingereza iliadhibu Estonia kwa kuikandika mabao matatu bila jawabu, nayo Italia ikaitia Lituania adabu kwa kipigo cha mabao mawili kwa nunge.

Ufaransa iliambulia bao moja kwa bila dhidi ya Georgia.