1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAMBURG: Uchunguzi wa miale ya nyuklia kaskazini ya Ujerumani

9 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCkr

Polisi nchini Ujerumani wamekuta dalili za miale ya nyuklia katika nyumba mbili mjini Hamburg.Nyumba hizo zinahusika na mtu aliewasiliana na Alexander Litvinenko,jasusi wa zamani wa Kirussi aliefariki mwezi uliopita kwa sumu ya miale ya nyuklia.Jana usiku polisi walikuta dalili za miale ya nyuklia katika fleti ya mfanyabiashara wa Kirussi Dmitry Kovtun aliekutana na Litvinenko mjini London,kabla ya jasusi huyo wa zamani kufariki hospitali.Siku ya Jumamosi,polisi waliarifu kuwa wamegundua ishara za miale katika nyumba nyingine nje ya mji wa bandari wa Hamburg.Kovtun ni mmoja kati ya Warussi wawili waliokutana na Litvinenko mjini London tarehe mosi Novemba.Ripoti zinasema yeye pia yupo hospitali mjini Moscow akipokea matibabu,baada ya sumu ya miale ya nyuklia kukutikana mwilini mwake.