1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamburg SV yajaribu bahati dhidi ya Bayern

20 Septemba 2014

Bayern Munich inasubiriwa na kikosi cha Hamburg SV kikiwa chini ya uongozi mpya leo jioni(20.09.2014)katika igi kuu ya Ujerumani Bundesliga.

https://p.dw.com/p/1DG29
Hambuger SV Johan Djourou Lewis Holtby Tolgay Arslan Fußball
Wachezaji wa Hamburg SV wakijadiliana uwanjaniPicha: picture alliance/dpa/Peter Steffen

Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola alibadilisha mtindo wake wa kucheza kwa mbinu ya mfumo wa 3-4-1-2 na kwenda katika mfumo wa 4-1-2-3 katikati ya mchezo ambao timu hiyo ilitoka na ushindi mwembamba nyumbani dhidi ya Manchester City , na mabadiliko hayo yalileta matunda , wakati Bayern ikicheza katika moja ya mchezo wake mgumu kabisa wa msimu huu, na kupata ushindi katika dakika ya 90 ambapo mlinzi Jerom Boateng alipachika bao la ushindi.

"Tulikuwa na matatizo kuudhibiti mpira , ndio sababu tulibadilisha kutoka ulinzi wa mabeki watatu na kuwatumia walinzi wanne," amesema Guardiola , ambaye hakutaka kusema atatumia mfumo gani dhidi ya Hamburg leo jioni(20.09.2014).

Fußball Champions League Gruppe E FC Bayern München Manchester City Pep Guardiola
Kocha wa Bayern FC Pep GuardiolaPicha: picture-alliance/dpa/Sven Hoppe

Hamburg ambayo iko mkiani mwa ligi ya Ujerumani Bundesliga ina matatizo yake binafsi, licha ya kuwa timu hiyo kutoka kaskazini mwa Ujerumani ina matumaini kwamba imetatua baadhi ya matatizo hayo kwa kumfuta kazi kocha Mirko Slomka baada ya kupata point moja tu na bila timu yake kufunga bao katika michezo mitatu ya ligi hiyo.

Kocha mpya ni kocha wa zamani wa kikosi cha vijana wa chini ya miaka 23 wa Hamburg Josef Zinnbauer.

Fußball, Bundesliga, 3. Spieltag, Hannover 96 - Hamburger SV
Kocha wa zamani wa Hamburg SV, Mirko SlomkaPicha: picture-alliance/dpa/Peter Steffen

Hali si swari kwa Hamburg

Hali si swari kwa Sinnbauer kwa kupambana na Bayern baada ya kupewa jukumu la kukiongoza kikosi hicho, ambaye ameitaja Bayern kuwa timu bora kabisa duniani., lakini ameongeza Hamburg haina cha kupoteza katika mchezo huo.

"Bayern ina nafasi kubwa ya kushinda katika mchezo huu na kwa hiyo tunaweza kujipiga kifua kwa kuwa hatuna cha kupoteza, na tutaangalia, tuna uwezo kiasi gani dhidi ya Bayern."

Viongozi wa ligi hiyo Bayer Leverkusen wanawania kuendeleza ubabe wao ambapo wanasafiri kwenda kukumbana na VFL Wolfsburg kesho Jumapili , wakati timu mbili ambazo zinamatumaini kwamba mashabiki wao wanaweza kusaidia hatimaye kupata ushindi msimu huu ni Schalke 04 na VFB Stuttgart, timu ambazo zina kibarua leo jioni dhidi ya Eintracht Frankfurt na Hoffenheim.

Kwa mujibu wa msimamo wa ligi wa mwanzoni mwa msimu , mchezo mzuri zaidi utakuwa kati ya kikosi kilichopanda daraja msimu huu SC Paderborn ikiikaribisha nyumbani Hannover 96 leo jioni.

Padeborn haijapoteza mchezo msimu huu na haijafungwa bao katika michezo miwili iliyopita.

Michezo mingine ni kati ya Ausburg ikipambana na Werder Bremen , na kocha wa makamu bingwa Borussia Dortmund , Juergen Klopp anarejea katika uwanja alioanzia kazi hiyo wa Mainz 05 jioni ya Jumamosi.

Achtelfinale Jürgen Klopp Jubel
Kocha wa Borussia Dortmund Jürgen KloppPicha: picture-alliance/augenklick/firo Sportphoto

Arsenal yataka kuondoa mkosi

Nchini Uingereza kocha wa Arsenal London Arsene Wenger atajaribu kuirejesha Arsenal katika njia ya ushindi dhidi ya Aston Villa leo baada ya wiki ya kufadhaisha.

Michezo mingine leo ni kati ya Newcastle inapambana na Hull City , West Ham United inamiadi na Liverpool, wakati kesho Manchester City wanaikaribisha Chelsea na Manchester United itaoneshana kazi na Leicester City.

Vipigo mara mbili mfululizo vimewaacha mabingwa wa Ulaya wa Champions League Real Madrid wakikabiliwa na mlima wa kupanda ikiwa ni michezo mitatu tu imefanyika katika La Liga iwapo inataka kuwakamata viongozi wa ligi hiyo kwa sasa Barcelona.

Cristiano Ronaldo UEFA Super Cup Madrid vs Sevilla
Picha: Getty Images

Real Madrid inakwaana na Deportivo la Coruna leo jioni(20.09.2014). Michezo mingine leo ni pamoja na Athletic Bilbao ikiikaribisha Granada, Atletico Madrid ina miadi na Celta Vigo na Espanyol inatiana kifuani na Malaga.

Jumapili Barcelona inasubiriwa nyumbani na Levante.

Mwandishi: Sekione Kitojo

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman