1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamburg: Polisi katika mji wa Hamburg, kaskazini ya hapa Ujerumani, ...

29 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFwl
wamesema wamemkamata raia wa Algeria anayeshukiwa kuhusika na ugaidi. Mwendeshaji mashtaka alisema mtu huyo wa kiume alikamatwa kwa ombi la wakuu wa Italy. Hiyo inasadifu na kukamatwa watu wanne wa kutokea Afrika Kaskazini nchini Italy. Washukiwa hao wanadaiwa kuwa walikuwa wakiwaandikisha watu wa kufanya mashambulio ya kujitolea mhanga nchini Iraq.
<br><br>
Pia polisi wa Uengereza wanasema wanamshikilia mwanamume mwenye umri wa miaka 33 baada ya kumkamata nyumbani kwake huko Birmingham, chini ya sheria ya kupambana na ugaidi. Juzi polisi wa Uengereza pia waliwakamata watu wawili huko Cloucester. Mmoja wao, mwenye umri wa miaka 24, inadaiwa alipatikana na baruti nyumbani kwake. Waziri wa mambo ya ndani, David Blankett, amesema watu hao wanashukiwa wana maingiliano na mtandao wa al-Qaida.