1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAMBURG : Mtambo wa nuklea hakuathirika

29 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnM

Polisi kaskazini mwa Ujerumani imesema lwamba mtambo wa kuzalisha umeme kwa njia ya nuklea haukuathirika baada ya kuzuka moto katika kituo cha umeme kilioko karibu.

Askari wa kuzima moto wameweza kuuzima moto huo.Maafisa wanasema hakuna hatari ya kuvuja kwa miale ya sumu za nuklea na bado haijulikani nini kilichosababisha moto huo kwenye kituo cha umeme cha Krümmel kilioko kama kilomita 30 kusini mashariki mwa mji wa Hamburg.

Tukio hilio limekuja masaa mawili baada ya mtambo mwengine wa kuzalisha umeme kwa nguvu za nuklea katika eneo hilo wa Bruntsbüttel kufungwa kwa tahadhari kutokana na kushika chaji mno.