1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamburg: Mounir al-Motassadeq, mshirika katika mashambulio ya kigaidi ya Septemba 11, 2001 nchini Marekani apewa kifungo cha miaka 15 hapa Ujerumani.

9 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CBHf

Mahakama ya hapa Ujerumani imezidisha hadi kiwango cha juu kabisa cha miaka 15 hukumu aliyopewa raia wa Moroko aliyepatikana na hatia ya kuhusika na mashambulio ya kigaidi ya Septemba 11, mwaka 2001 huko Marekani. Mounir al-Motassadeq alihukumiwa kwanza kifungo cha miaka saba gerezani hapo Novemba mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kuujua mpango wa kuuliwa abiria 246 wa ndege pamoja na marubani katika mashambulio ya Septemba 11. Pia alipatikana na hatia ya kuwa mwanachama wa jumuiya ya kigaidi. Hii ilikuwa kesi ya tatu kwa Motassadeq ambaye ni mtu wa kwanza kuwahi kupatikana na hatia ya mashambulio ya Septemba 11 mwaka 2001. Wakili wa Mounir al-Motassadeq, Bwana Ladislav Anisic, baada ya kutolewa hkumu hiyo alisema:

+Nini tutakachofanya ni rahisi, kukata upya rufaa. Malalmiko yako njiani kwamba katiba imeendewa kinyume. Tunatayarisha kutaka kesi isikilizwe upya, na mengi mengine. Bado tuna hoja za kuipinga hukumu hiyo.+