1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAMBURG: Motassadeq apewa kifungo cha miaka 7

20 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEjP

Mahakama mjini Hamburg,kaskazini mwa Ujerumani,imetoa adhabu ya kifungo cha miaka 7 kwa Mmorokko,Mounir el-Motassadeq alieshtakiwa kuwa na mahusiano na kundi la kigaidi.Lakini Motassadeq hajakutikana na hatia katika mashtaka mengine ya kuhusika na mauaji katika mashambulio ya Septemba 11 mwaka 2001.Miaka miwili iliyopita Motassadeq alikutikana na hatia kwa mashtaka yote mawili,lakini mwaka jana alipokata rufaa,uamuzi huo ulibadilishwa.Matokeo ya kesi hiyo yalitegemea kwa sehemu kubwa ushahidi uliotoka kwa wafungwa waliokuwa wafuasi wa al-Qaeda na wamezuiliwa na Marekani.Serikali ya Marekani haikuwaruhusu wafungwa hao kutoa ushahidi katika kesi ya mwanzo.Mahakama ya Hamburg katika kesi ya pili ilipewa nakala za mahojiano yaliofanywa pamoja na watuhumiwa.