HAMBURG: Mchango wa NATO uimarishwe Afghanistan
24 Septemba 2006Matangazo
Katibu Mkuu wa Shirika la Kujihami la NATO,Jaap de Hoop Scheffer ametoa wito kwa shirika hilo kupanua ujumbe wake nchini Afghanistan.Kwa mujibu wa makala iliyochapishwa na gazeti la Kijerumani “Bild am Sonntag,” De Hoop amesema,Afghanistan kamwe isiwe tena kambi ya kutoa mafunzo kwa magaidi.Siku moja kabla ya bunge la Ujerumani kupiga kura ikiwa irefushe mamlaka ya kubakia na vikosi vya amani nchini Afghanistan,De Hoop ameitaka serikali ya Berlin itoe mchango zaidi katika vikosi vya kimataifa nchini Afghanistan.