1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamburg. Mawaziri wasigana juu ya upunguzaji wa gesi zinazoharibu mazingira.

30 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwp

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa bara la Asia na Ulaya wanaokutana mjini Hamburg , nchini Ujerumani wamesigana juu ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa. Waziri wa mambo ya kigeni wa China Yang Jiechi amesema kuwa punguzo kubwa katika gesi zinazoharibu mazingira ni lazima litoke katika mataifa yenye viwanda, lakini China itafanya kile inachokiweza.

China inaukuaji mkubwa wa kiuchumi, pamoja na kiwango kikubwa cha uchafuzi wa mazingira.

India imesema haitoweza kujifunga na malengo maalum ya utoaji wa gesi hizo kwasababu hali hiyo itarudisha nyuma kasi ya ukuaji wa uchumi inayohitajika kuitoa sehemu kubwa ya jamii kutoka katika umasikini.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, ambaye ni mwenyekiti wa mkutano huo , amesema mataifa hayo 43 yamekubaliana kuwapo na mpango wa ufuatiliaji baada ya kumalizika kwa muda wa makubaliano ya Kyoto mwaka 2012. Tofauti juu ya kupambana na ujoto duniani zitaingia katika mkutano wa mataifa tajiri yenye viwanda duniani G8 wiki ijayo.