1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamburg kugombea nafasi ya kuandaa Olimpiki 2024

13 Machi 2015

Mji wa bandari wa kaskazini mwa Ujerumani Hamburg umeupiku mji mkuu Berlin katika kinyang'anyiro chao cha kuwa mgombea wa Ujerumani wa kuandaa Michezo ya Olimpiki ya 2024

https://p.dw.com/p/1EqXL
Deutschland Forsa-Umfrage
Picha: picture alliance/dpa/Daniel Reinhardt

Hamburg imepata uungwaji mkono kutoka kwa idadi kubwa ya wakaazi wake katika uchunguzi wa maoni. Shirikisho la Michezo ya Olimpiki la Ujerumani – DOSB limesema Hamburg itawasilisha ombi rasmi kwa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki IOC.

Miji ya Boston na Roma pia imetangaza maombi yao ya kugombea uwenyeji huku miji mingine kadhaa ikiwemo Budapest, Istanbul, Doha, Baku na Paris ikitafakari kutuma maombi yao.

Muda wa mwisho wa kuwasilisha maombi ya kugombea uwenyeji ni Septemba ambapo Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki - IOC itatangaza mshindi mwaka wa 2017. Rio de Janeiro itaandaa Michezo ya Olimpiki 2016 wakati Tokyo ikiandaa tamasha hilo 2020

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters
Mhariri:Gakuba Daniel