1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAMBURG. China kufanya mageuzi katika sekta ya biashara

14 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDCQ

Waziri mkuu wa China Wen Jiabao amesema kuwa nchi yake itachukua hatua madhubuti za kulinda haki za kimataifa juu ya mali na biashara.

Wen Jiabao ameyasema hayo alipohudhuria mkutano mkuu wa kibiashara wa siku tatu uanoendelea katika mji wa Hamburg kaskazini mwa Ujerumani.

Waziri mkuu wa China pia amedokeza kuwa nchi yake itajihusisha zaidi na mageuzi katika sekta ya kibiashara.

Wen Jiabao yuko nchini Ujerumani kwa ziara ya siku mbili ambayo pia anatarajiwa kukutana na kansela wa Ujerumani bibi Angela Merkel kujadili juu ya maswala muhinu ya kimataifa likiwemo swala la mashariki ya kati na kuishawishi Iran iache mpango wake wa nyuklia.

China ni mshirika mkuu wa kibiashara wa Ujerumani, biashara baina ya nchi mbili hizi imefikia thamani ya Euero billioni 61.2.