1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamasa ya kujikinga na Corona bado chini Tanzania

9 Julai 2021

Wakati Tanzania inakabiliwa na wimbi la tatu la mripuko wa virusi vya Corona, hamasa ya kujikinga na janga hilo bado iko chini ikilinganishwa na wakati nchi hiyo ilipokumbwa na wimbi la kwanza na lile la pili.

https://p.dw.com/p/3wGfd
Tansania Dar es Salaam Coronavirus
Picha: DW/E. Boniphace

Wakati Tanzania inakabiliwa na wimbi la tatu la mripuko wa virusi vya Corona, hamasa ya kujikinga na janga hilo bado iko chini ikilinganishwa na wakati nchi hiyo ilipokumbwa na wimbi la kwanza na lile la pili. Moja ya eneo hatari ni msongamano mkubwa kwenye vyombo vya usafiri. 

Mtizamo huo unaonyeshwa na watu wa makundi mbalimbali ambao kwa Nyakati tofauti wamesema kuwa hamasa ya kujikinga na wimbi la kwanza la COVID 19 na lile la pili ilikuwa kubwa ikilingishwa na sasa.

Wakizungumza na Idhaa hii ya kiswahili ya DW kwa nyakati tofauti watu kutoka katika makundi mbalimbali nchini Tanzania, wanasema kuwa hamasa ya kujikinga na janga hilo la Covid-19 katika wimbi la tatu inaonekana kuwa ndogo huku baadhi ya watu wakionekana kutokuchukua tahadhari zinazoelekezwa na wataalam wa afya nchini humu. Bwana Ntakije Ntanena mkaazi wa Kigoma anasema hali anayo ina hivi sasa ni tofauti na mripuko wa kwanza na ule wa pili.

Uganda Unterschrift EACOP in Kampala
Rais Samia amewahimiza wananchi kuchukua tahadhariPicha: Presidential Press Unit/Uganda

Akiwa ziarani mkoani Morogoro hivi karibuni Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alisisitiza kuwa Tanzania inakabiliwa na wimbi la tatu la Covid-19 na hivyo kuwataka watu kuzingatia maelekezo ya wataalam wa afya ikiwemo uvaaji wa barakoa.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii nchini Tanzania, wanasema Watanzania wanapaswa kujifunza katika wimbi la kwanza na la pili ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari kubwa katika kupambana na vita hii inavyoonekana kuwa pasua kichwa ulimwenguni kote. Gwandumi Mwakatobe ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii akiwa Sumbawanga mkoani Rukwa.

Wakati hayo yakichomoza kwa upande mwingine Mwenyekiti wa chama cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, Free Man Mbowe ameweka wazi kifo cha kaka yake Charles Alikael Mbowe kuwa kimetokana na ugonjwa wa COVID-19 na kuongeza kuwa.

Nchi ya Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki zinazokabiliwa na wimbi la tatu la Covid-19 hivi sasa huku Serikali ya nchi hiyo ikionekana kuchukua hatua ikiwemo kukamilisha mchakato wa chanjo kwa wananchi wake watakao kuwa tayari kuchanjwa.

Deo Kaji Makomba, DW Dodoma