Hamas na Fatah watia saini makubaliano ya umoja, Beijing
23 Julai 2024Matangazo
Chombo hicho kilieleza azmio hilo pia linaatilia mkazo kustawisha umoja wa Wapalestina. Hatua hiyo imefikwa katika kipindi ambacho Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken akisema kuna ishara ya usitishwaji mapigano kati ya Israeli na Hamas.
Makundi hayo mawili hasimu ya Kipalestina, pamoja na mengine 12 ya kisiasa, walikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, kuhitimisha mazungumzo hayo yalianza Jumapili.
Hamas na Mamlaka ya Palestina wamekuwa na duru nyingi za mazungumzo ya umoja zilikuwa zinafeli tangu Hamas ilipovitimua vikosi vya Fatah kutoka Gaza katika unyakuzi mkali wa eneo hilo mwaka 2007.