SiasaUkraine
EU yapendekeza vikwazo vipya dhidi ya Urusi
16 Novemba 2023Matangazo
Pendekezo hilo linajumuisha vikwazo dhidi ya watu 120 zaidi pamoja na taasisi kwa jukumu lao katika kuhujumu uhuru na uadilifu wa kimaeneo wa Ukraine. Pendekezo hilo pia linajumuisha vikwazo vipya vya kuagiza na kusafirisha bidhaa nchini Urusi, pamoja na hatua za kudumisha ukomo wa bei ya mafuta na kukabiliana na ukwepaji wa vikwazo hivyo vya Umoja wa Ulaya.
Wanaopendekezwa kuwekwa chini ya vikwazo vipya
Wanaopendekezwa kuorodheshwa chini ya vikwazo hivyo vipya ni pamoja na maafisa kutoka jeshi la Urusi, sekta za ulinzi na teknolojia ya habari pamoja na wadau muhimu wa kiuchumi.
Wawakilishi wa mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya wanatathmini pendekezo hilo la vikwazo vipya vinavyopaswa kutekelezwa ifikapo mwisho wa mwaka .