Hali ya kiusalama imekuwa mbaya katika siku za hivi karibuni huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo jeshi la taifa nchini humo FARDC limekuwa likipambana na waasi wa M23 hasa katika mji wa Sake uliopo takriban kilometa 27 kutoka mji wa Goma. Bakari Ubena amezungumza na Reagen MIVIRI, mtafiti na mchambuzi wa masuala ya usalama katika shirika la Congo Research Group.