Hali ya kisiasa nchini Kenya baada ya mawaziri kusimamishwa kazi
16 Februari 2010Mabishano yaliotokea huko Kenya kati ya Rais Mwai Kibaki wa nchi hiyo na waziri mkuu Raila Odinga juu ya kufukuzwa kazi mawaziri wa kilimo na elimu, William Ruto na Samuel Ongeri, yametapakaa na kuleta hofu kwamba serikali ya sasa ya muungano kati ya vyama vya PNU na ODM huenda ikaporomoka na kupelekea kuitishwa uchaguzi mkuu wa mapema. Hii ni kwa mujibu wa wakili mkuu wa serikali ya Kenya, Amos Wako. Katika mji wa Eldoret usalama umeimarishwa na polisi kufuatia kitisho cha kufanywa maandamano ya kumpinga Raila Odinga kwa uamuzi wake wa kutaka kumsimamisha kazi waziri William Ruto.
Othman Miraji alizungumza na waziri wa utalii wa Kenya, Najib Balala, kwa njia ya simu punde hivi, na kumuuliza malumbano haya baina ya Rais Kibaki na waziri mkuu Odinga yanaipeleka Kenya wapi?
Mahojiano: Othman Miraji/Najib Balala Mhariri: Mohamed Abdulrahman