Hali ya hewa:
18 Novemba 2007Matangazo
VALENCIA:
Wataalamu wa sayansi wa kikundi cha serikali mbali mbali juu ya badiliko la hali ya hewa (ICC) wametoa onyo lao kali kabisa juu ya kuzidi ujoto katika sayari yetu.Ripoti yao mpya iliotolewa huko Valencia,Spain, hapo jana imesema ujoto unaosababishwa na kuunguza petroli unazidi haraka zaidi kuliko ilivyodhaniwa kabla na athari zake huenda zizuilike tena.
Katibu mkuu wa UM Ban Ki-moon, aliwaambia wajumbe :
„Serikali zapaswa kuhimiza maafikiano katika mkutano ujao wa mabadiliko ya hali ya hewa utakaofanyika kisiwani Bali,Indonesia mwezi ujao.
Kamishna wa Umoja wa Ulaya anaehusika na maswali ya mazingira Stavros Dimas ameieleza ripoti ya wanasaynasi hao ni ya kihistoria.