Hali ya hewa yakwamisha safari, Ulaya.
25 Desemba 2010Takriban ndege 400 katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle mjini Paris ziliahirisha safari zake jana jioni na nyingine kuchelewa, hali iliyowaacha maelfu ya wasafiri kuvuruga ratiba zao za kusherehekea sikukuu hii ya leo.
Maafisa nchini Ufaransa wamesema walitowa mahitaji ya dharura kama vile vitanda na mablangeti kwa wasafiri hao waliokwama.
Tatizo la ndege kuahirisha safari zake pia limesababishwa na uhaba wa maji yanayotumika kuyayusha barafu kwenye ndege , uhaba ambao ulisababishwa na mgomo katika viwanda vinavyotengeneza maji hayo.
Nchini Ujerumani huduma za treni kati ya mji wa Berlin na Hanover ilisimama kutokana na hali ya baridi kali hapo jana na kusababisha abiria takriban 700 kukwama kwa saa kadhaa ndani ya treni.