Hali ya afya ya rais Buhari nzuri
16 Februari 2017Matangazo
Bukola Saraki jana alikwenda katika mji mkuu wa Uingereza pamoja na kiongozi wa wajumbe walio wengi katika baraza la Seneti, Ahmed Lawan, na spika wa baraza la wawakilishi, Yakub Dogora. Ni ujumbe wa hivi karibuni kabisa wa kisiasa kumtembelea kiongozi huyo mwenye mri wa miaka 74 katika makaazi rasmi ya ubalozi wa Nigeria nchini Uingereza, ambako amekuwa akiishi kwa karibu mwezi mmoja. Saraki amesema katika taarifa kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Facebook kwamba Buhari yuko katika hali nzuri kiafya, na hakuna sababu ya wasiwasi. Katika ukurasa wa Twitter Buhari ameandika jana kwamba amefurahishwa na ziara hiyo na kuwashukuru Wanigeria, Wakristo na Waislamu kwa dua zao na kumtakia kheri ya afya njema.