Hali mbaya ya hewa yasababisha watoto kupoteza makazi
6 Oktoba 2023Hayo ni kulingana na ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Watoto UNICEF ambalo limesema majanga hayo yaliyochochewa na mabadiliko ya tabia nchi ni pamoja na mafuriko, ukame, vimbunga na moto wa misituni.
Kulingana na ripoti hiyo, mafuriko na vimbunga vilisababisha asilimia 95 ya makaazi yaliyopotezwa.
Laura Healy, mtafiti mwenza wa ripoti hiyo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba ilikadiriwa kuwa takriban Watoto 20,000 walilazimika kuyakimbia makaazi yao kila siku.
Hali hiyo inaonesha jinsi watoto walioathiriwa wako katika hatari ya kukumbwa na matatizo zaidi, kama vile kutengwa na wazazi wao au kuwa waathirika wa walanguzi wa watoto.
Wataalamu wametahadharisha kuwa katika miaka 30 ijayo, mafuriko yanaweza kusababisha watoto milioni 96 kuhama makaazi yao.