1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haley asema sera ya utengano sio nzuri kwa Marekani

24 Agosti 2024

Balozi wa zamani wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley, amesema sera ya utengano haina manufaa na kutoa wito kwa nchi yake kusimama pamoja na washirika wake, ameyasema hayo katika ziara yake Taiwan.

https://p.dw.com/p/4jsRC
Marekani | Nikki Haley
Balozi wa zamani wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki HaleyPicha: Kyodo/picture alliance

Akizungumza na waandishi habari mjini Taipei,  Haley amesema uungaji mkono wa washirika wake wakiwemo Ukraine na Israel ni muhimu huku akisisitiza  pia umuhimu wa Taiwan kisiwa kinachojitawala chenyewe ambacho China inadai kuwa sehemu ya himaya yake kutaka kuidhibiti kikamilifu. 

Haley amesisitiza umuhimu wa Washington kushirikiana na Taipei akisema ni bora kufanya kazi na rafiki wa Marekani kuliko maadui

"Afadhali nifanye biashara na marafiki zetu kuliko kufanya biashara na maadui zetu. Kwa hiyo, nitasema wazi kwamba ushirikiano wa uzalishaji wa chip ambao tunao kati ya Marekani na Taiwan sio iliyo na nguvu pekee ni kitu tunachohitaji kuishamrisha zaidi ushirikiano wetu, nadhani pia sio suala la kuitaka Tauiwan kulipia ulinzi wao, Taiwan imeagiza vifaa zaidi vya kijeshi, tunahitaji kuongeza ushirikiano wetu katika mafunzo nao, na tunapaswa kuhakikisha kuwa Taiwan ni kipaumbele chetu tunapowapa vifaa wanavyohitaji,” alisema Haley.

Kiongozi wa Taiwan asema China haina haki ya ´kuwaandama´

Marekani bado haijaitambua rasmi Taiwan kama kisiwa huru lakini inakiunga mkono na ndio mshirika mkuu wa kuiuzia silaha.