1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi Afghan yaumwa Mjerumani mmoja na Mlinzi

22 Mei 2017

Wakati habari ya kushitua ya mashambulizi dhidi ya shirika la misaada la Sweden ilipotufika, tulikuwa tupo katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, tukiwa tumekaa na wakimbizi kutoka Afghanistan ambao walirudishwa

https://p.dw.com/p/2dNHo
Afghanistan Birgitta Schülke-Gill und Sandra Petersmann in Kabul
Picha: DW

Tunaendelea na kazi zetu, kusikiliza na kusoma ripoti za watu wanaorudishwa makwao. Amir, Nuri, Mujtaba na Isa wanatuambia wanaishi kwa hofu juu maisha yao mijini Kabul.

Tulipata mshituko na kupigwa na bumbuwazi. Mashambulizi yote ni ya kushitua. Kabul, Paris, Brussels, Nice na Berlin. Na maelezo mpaka leo hayajawa ya kufahamika.

Tumewasiliana na watu wetu Kabul ili kupata maelezo zaidi. Tunafuta kile kinachoripotiwa katika mitandao ya kijamii na wafanya kazi wenzetu waliokuwepo Afghanistan.

Tunajaribu kuzijulisha familia zetu kuwa tuko sawa. Marafiki na wafanyakazi wenzetu wanapiga simu au kutuma ujumbe kupitia WhatsApp. Wakimbizi waliorudishwa kutoka Ujerumani wanafahamu Kijerumani kiasi cha kuweza kufahamu mazungumzo yetu na watu nyumbani. Mujtaba na Isa wametupa pole. Tunazungumza na mhariri mkuu na mratibu wa usalama na tunaizingatia hali hii vizuri sana.

Hali sasa inaanza kufahamika. Mashambulizi ya Jumamosi yalikusudiwa wageni. Na lengo kubwa lilikuwa ni kulishambulia jengo la shirika la misaada. Mlinzi kutoka Afghanistan na Mjerumani aliyekuwa akifanya kazi katika shirika hilo la misaada waliuwawa. Mlinzi alikatwa kichwa na mfanyakazi mmoja kutoka Finland alitekwa nyara.

Sio mara ya kwanza kutokea mashambulizi dhidi ya wageni mjini Kabul. Lakini mara nyingi waathirika huwa wenyewe Waafghani. Kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu, kumekuwa  na mashambulizi saba mjini Kabul ambayo zaidi ya watu 100 waliuwawa na kujeruhiwa. Washambuliaji ni kundi la Taliban au kundi lijiitalo Dola la Kiislam (IS).

Mji mkuu wa Afghanistan umetulia kidogo siku hizi. Tulipotua mjini Kabul siku chache zilizopita, mji ambao umezungukwa na kuta na waya kwa ajili ya ulinzi na usalama, unaonekana kuwa mji wa amani. Jua liliwaka sana na mawingu ya buluu. Watu wa mji huu ambao tumekuwa tukizungumza nao ni wakarimu. Lakini kwa mashambulizi haya ya hivi karibuni, inaonesha kuwa hakuna utulivu wala amani hapa.

Hakuna uhakika wa usalama mjini Kabul. Pahala ambapo pana usalama sasa panaweza kushambuliwa kesho. Kabla ya sisi kuondoka, lazima tuzingatie na tufuate hatua za usalama wetu ambazo tumejiwekea wenyewe. Tunasikiliza nafsi zetu.

FIKRA ZA WATU JUU YA KUONGEZWA MAJESHI AFGHAN

Tumewauliza watu wengi, wanafikiria nini juu Marekani na wanachama wengine wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO kutaka kuongeza majeshi nchi Afghanistan.

"Kitendo hicho hakitasaida lolote. Kitu muhimu ni kuwa sisi Waafghani tuungane na tusimame pamoja, na serikali yetu ianze kuongoza badala ya kubishana."

"Majeshi ya kigeni yatasaidia nini ikiwa hawaruhusiwi kupigana?"

"Lazima tuondoe majeshi yote ya nje na tuunge mkoni majeshi yetu."

"Jumuiya ya Kujihami ya NATO haijafanikiwa hapa."

"Watuletee majeshi ya usalama ya Umoja wa Mataifa."

"Tunachokitaka kutoka jumuia ya kimataifa ni usalama kwanza halafu ndio elimu."

Kuna majibu mbali mbali, lakini watu wote tuliozungumza nao wakiwa wanaume au wanawake hakuna aliyejihisi kuwa salama mjini Kabul, bali wanaendelea kuishi kwa hofu na maisha yanasonga mbele. Mara nyingi tunasikia watu wakisema: "Tukitoka majumbani kwetu, hatujui kuwa jioni tutarudi hai au la, lakini hatuwezi tukasimamisha maisha yetu. Lazima tuendelee na shughuli zetu."

Tukiwa kama wageni kutoka nje, mjini Kabul usalama wetu haujabadilika sana baada ya mashambulizi haya.  Ugaidi na migogoro hapa ni sehemu ya maisha ya kila siku, na pia migogoro ya makundi mbalimbali ya uhalifu. Kutekwa nyara hapa Kabul ni sehemu ya biashara.

Sisi tupo hapa kama waandishi wa habari. Tunaonesha hali halisi ya maisha ya kila siku ya mji mkuu huu wa Kabul. Tunaijua nchi hii vizuri kwa sababu tumeshakuja sana hapa. Afghanistani ni nchi ya vita.

Tangu kuletwa kwa majeshi ya kimataifa, sasa ni miaka 16, hili limeleta maendeleo na kuifungua nchi zaidi, lakini wanajeshi hawa hawajaleta amani wala usalama.

Mwandishi: Sandra Petersmann, Birgitta Schülke-Gill

Tafsiri: Najma Said

Mhariri:  Mohammed Khelef