Hakuna kugawana mali nusu kwa nusu baada ya talaka
15 Mei 2018Mahakama kuu nchini Kenya imekataa ombi la kubadilishwa kwa sheria ili kuruhusu wanandoa kugawana mali yao nusu kwa nusu wakati wa talaka. Wanaharakati wamesema uamuzi huo ni pigo kwa haki za wanawake nchini humo. Chama cha wanawake mawakili wa Kenya FIDA ambacho pia kinatetea haki za wanawake kiliwasilisha ombi mahakamani mwaka 2016, kikisema kuwa kipengee cha mali ya wanandoa ni kinyume na sheria kwa kuwa kilimpa mwanandoa umiliki wa mali tu ambayo alileta. Chama hicho kilisema kuwa katiba ya Kenya inasema wanandoa wana haki sawa hivyo kipengee hicho kinawaathiri wanawake ambao wanaweza kupatwa na hasara ya fedha wakati ndoa inapovunjika. Katika uamuzi wake, mahakama hiyo ilisema kubadilisha sheria hiyo kutafungua mlango kwa mtu kuingia katika ndoa na apate mali nyingi kuliko anayostahili kupata wakati wa talaka