Haki za wenyeji asilia Australia
13 Februari 2008Hatua ya waziri mkuu huyo imefungua ukurasa mpya katika uhusiano baina ya wanyeji hao na serikali ya Australia.
Akizungumza bungeni,kuwaomba radhi rasmi wenyeji asilia wa Australia, waziri Mkuu Rudd amesema mjini Canberra kuwa sheria na sera za nchi zilisababisha, uchungu na maonevu kwa watu hao ,kwa muda wa miaka mingi.
Amesema samahani kwa watu hao ,kwa mateso na dhulma iliyowafika.
Waziri Mkuu Rudd amesema wakati sasa umefika wa kufungua ukarasa mpya katika historia ya Australia kwa kusahihisa makosa waliyofanyiwa wenyyeji wa nchi hiyo, ili kuweza kusonga mbele kwa nia safi.
Katika hotuba yake waziri mkuu huyo pia aliomba samahani kwa niaba ya mabunge na serikali zilizopita nchini Australia kwa kutekeleza sera zilizosababisha maonevu makubwa kwa wakazi asilia wa nchi hiyo.