1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haiti yakabiliwa na uhaba wa bidhaa za matibabu

10 Aprili 2024

Milio ya risasi imesikika upya katikati mwa mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince na kuwalazimisha wafanyikazi wa misaada kusitisha kwa haraka shughuli zao zinazohitajika na maelfu ya raia wa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4ebvb
Haiti- Port-au-Prince
Hali inazidi kuwa mbaya kila siku nchini Haiti Picha: Odelyn Joseph/AP Photo/picture alliance

Shirika la msaada wa kibinadamu la The Alliance for International Medical Action, lenye makao yake nchini Senegal, limeonya kuwa wiki kadhaa za ghasia za magenge nchini humo, zimesababisha kufungwa kwa hospitali 18 na pia kuchangia uhaba wa bidhaa za matibabu kutokana na kufungwa kwa bandari kubwa na uwanja wa kimataifa wa ndege.

Antoine Maillard mratibu wa shirika hilo la The Alliance for International Medical Action mjini Port-au-Prince, amesema hali inazidi kubadilika na kuathiri shughuli za shirika hilo kila siku.

Viongozi wa Haiti wakubaliana kuunda serikali ya mpito

Maillard ameongeza kuwa wafanyakazi wa msaada waliweza kufikia kambi moja ya wakimbizi hapo jana lakini milio hiyo ya risasi ilizuia kutolewa kwa msaada katika kambi hiyo.

Maillard amesema dawa zinazopatikana kwa sasa zimepanda bei maradufu.