Hailemariam awasili Cairo kwa mazungumzo ya mto Nile
17 Januari 2018Matangazo
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn amewasili mjini Cairo kwa ziara ya siku mbili kujadili ujenzi wa bwawa kubwa linalojengwa na Ethiopia katika mto Nile na ambalo Misri inahofia kwamba litachukua sehemu yake ya mto huo.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imesema leo katika taarifa yake kwamba Desalegn atakutana na Rais wa Misri Abdel-Fattah el-Sissi kesho, na kwamba mawaziri wa kigeni wa mataifa hayo mawili walikutana kabla ya ziara hiyo.
Misri imekuwa ikionesha wasiwasi juu ya ujenzi wa bwawa hilo ambalo linaelekea kukamilika karibuni. Mto Nile ni chanzo cha maji safi kwa idadi jumla ya watu milioni 95 wa Misri.
Ethiopia ambayo ina idadi sawa na hiyo, imesema bwawa hilo ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi ya nchi yake.