1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haftar awaamuru wanajeshi wake kupambana vikali

6 Mei 2019

Khalifa Haftar ambaye ni kamanda wa vikosi vya kijeshi vya mashariki mwa Libya amewataka wanajeshi wake kupambana vikali katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.

https://p.dw.com/p/3HzKk
Russland Moskau General Khalifa Haftar aus Libyen
Picha: picture-alliance/dpa/M. Shipenkov

Kamanda wa vikosi vya kijeshi vya mashariki mwa Libya, Khalifa Haftar, amewataka wanajeshi wake wanaojaribu kuukamata mji mkuu Tripoli kupambana vikali na kuwaangamiza maadui wao, akidai kuwa mwezi mtukufu wa Ramadhan ulioanza tarehe sita Mei, ni mwezi wa vita vitakatifu.

Kauli zake zimekuja saa chache tu baada ya Umoja wa Mataifa kutoa wito wa kuweka chini silaha kwa wiki nzima kwa misingi ya kiutu kufuatia mapigano ya mwezi mzima katika mji huo ambayo yamesababisha watu 50,000 kupoteza makazi na karibu 400 kuuawa pamoja na uharibifu mwingine mkubwa.

Jeshi la Haftar linalojiita Libyan National Army - LNA ambalo linaegemea serikali pinzani ya mashariki mwa nchi hiyo, halijaweza kuvunja ngome za kusini mwa Tripoli, ambao unadhibitiwa na serikali inayotambuliwa kimataifa.