1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres kwenda Misri

Josephat Charo
18 Oktoba 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anatarajiwa kusafiri kwenda nchini Misri huku mzozo wa kibinaadamu ukiendelea kuwa mbaya katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4Xeo0
USA, New York | Guterres auf einer Pressekonferenz im UN Hauptquatier
Picha: Craig Ruttle/AP/picture alliance

Taarifa hii imeripotiwa na gazeti la Financial Times likiwanukuu watu walio karibu na suala hilo.

Ripoti ya gazeti hilo imesema Guterres anatarajiwa kuwasili mjini Cairo mapema siku ya Jumatano (Oktoba 16) na atakutana na maafisa wa Misri akiwemo rais wa nchi hiyo, Abdel Fattah Al-Sisi.

Soma zaidi: Watu 25 wauawa katika mapigano ya Israel na wapiganaji wa Gaza

Wakati haya yakiarifiwa Waziri wa Mambo ya Nje ya Afrika Kusini Maledi Pandor amesema amezungumza na mkuu wa kundi la Hamas, Ismail Haniyeh, kujadili kuepeleka msaada kwa Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na maeneo mengine ya Wapalestina.

Pandor amekanusha madai ya kuunga mkono shambulizi la Hamas dhidi ya Israel.