1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres kufunguwa Mkutano wa Usalama wa Munich

16 Februari 2024

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anatarajiwa kufunguwa rasmi Mkutano wa 60 wa Kimataifa wa Usalama mjini Munich nchini Ujerumani ambapo viongozi 50 wanatazamiwa kuhudhuria hafla hiyo ya mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4cSy8
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.Picha: Gian Ehrenzeller/KEYSTONE/picture alliance

Mada kuu za mkutano huo ni mapigano yanayoendelea nchini Ukraine na vita vya Israel katika Ukanda wa Gaza.

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris anatarajiwa kuhutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa siku tatu.

Siku ya Jumamosi (Februari 16), Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani na Rais Voldymyr Zelensky wa Ukraine pia wanatarajiwa kuhutubia mkutano huo.

Soma zaidi: Urusi, Iran hazikualikwa Mkutano wa Usalama wa Munich

Rais Isaac Herzog wa Israel na waziri wake wa mambo ya nje, Israel Katz, pia wanatarajiwa kuhudhuria pamoja na wawakilishi wa ngazi za juu kutoka Mamlaka ya Palestina, Saudi Arabia, Qatar, Misri na Jordan.

Suala muhimu linalotarajiwa kujadiliwa pembezoni mwa mkutano huo ni matokeo ya uchaguzi wa Novemba 5 nchini Marekani na nini kitakachotokea ikiwa rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, atachaguliwa tena.