Guterres amependekeza njia ya kusafirisha nafaka ya Ukraine
25 Aprili 2023Matangazo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amependekeza kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin njia inayolenga kuuboresha mpango wa usafirishaji salama wa nafaka katika Bahari Nyeusi. Wizara ya ulinzi ya Urusi imeilaumu Ukraine kwa kujaribu kuzishambulia meli zake katika bahari hiyo. Imesema hatua hiyo inatishia makubaliano ya kusafirisha nafaka nje ya nchi. Wakati huo huo Rais wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev amesema ikiwa nchi za G7 zitaweka vikwazo kwenye shughuli za usafirishaji kwenda Urusi, basi nchi yake itajibu kwa kusitisha mara moja mpango wa kusafirisha nafaka za Ukraine katika Bahari Nyeusi. Urusi tayari imeashiria kuwa haitaruhusu kuendelea kwa usafirishaji huo baada tarehe 18 mwezi ujao wa Mei.