1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres aisifia Somalia kuanza kujijenga kitaasisi

21 Mei 2019

Katibu  mkuu wa Umoja  wa  Mataifa Antonio Guterres amesema Somalia inapiga  hatua  kuelekea ujenzi wa taifa lenye taasisi  imara.

https://p.dw.com/p/3Ip5N
Somalia Mogadischu - U.N. Generalsekretär Antonio Guterres bei Pressekonferenz
Picha: Reuters/F. Omar

Hata hivyo, Guterres alisema kuwa inabidi serikali ya Somalia ipambane na watu wenye itikadi kali wanaotumia nguvu, ugaidi, makundi yenye silaha, hali tete ya  kisiasa na rushwa.

Aliyasema hayo katika ripoti iliyowasilishwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kusambazwa  siku ya Jumatatu (Mei 21) kwamba changamoto hizo zinaonesha udhaifu wa hatua zilizopigwa hadi sasa na kutishia maendeleo zaidi.

Baada ya miongo mitatu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, mashambulizi ya watu wenye itikadi kali na  njaa, Somalia imeweza kuwa na serikali kamili mwaka 2012 na  hadi sasa imekuwa ikifanyakazi kujenga hali thabiti.