1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gulu, Uganda. LRA wakana kuuwawa kwa Otti.

7 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79D

Maafisa wa kundi la waasi la Lord’s Resistance Army , LRA wamekana leo kuwa kiongozi wa kundi hilo Joseph Kony amehusika kumuua naibu wake, wakikana ripoti za vyombo vya habari vya nchi hiyo kuwa kiongozi huyo namba mbili wa kundi hilo la waasi ameuwawa.Viongozi hao wote wawili wanatakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa makosa ya uhalifu wa kivita katika wakati wa miaka 20 ya mapigano na wameendelea kujificha katika maeneo ya msituni ya kaskazini mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo DRC, wakihofia kukamatwa iwapo watahudhuria mazungumzo ya amani. Vincent Otti , naibu mkuu wa kundi la LRA amekuwa akizungumza na wapatanishi na waandishi wa habari kila mara kupitia simu yake ya satalite kutokea katika maeneo ambayo hayafahamiki. Lakini amekuwa kimya katika wiki za karibuni na hapatikani katika simu zake kadha. Martin Ojul , raia wa Uganda ambaye anaishi uhamishoni ambaye pia ni mwakilishi wa ngazi ya juu wa uongozi wa LRA katika mazungumzo ya amani kusini mwa Sudan , amesema kuwa Otti , ambaye amekuwa sauti ya kundi hilo tangu msemaji wake wa mwanzo kujisalimisha mwaka 2005, ni mgonjwa.