Guinea yaadhimisha miaka 60 ya Uhuru
2 Oktoba 2018Matangazo
Guinea leo inaadhimisha miaka 60 ya Uhuru. Taifa hilo liliukataa ukoloni wa Ufaransa katika kura ya maoni lilipopiga kura kwa wingi kura ya Hapana Septemba 28 mwaka 1958 chini ya uongozi wa Rais Ahmed Sekou Toure.
Kutokana na uamuzi huo, Oktoba mbili mwaka 1958, siku mbili baada ya kura ya maoni Guinea ikawa rasmi taifa huru, likiwa la kwanza miongoni mwa makoloni ya Ufaransa barani Afrika na la pili baada ya Ghana iliojinyakulia Uhuru kutoka kwa Uingereza 1957.