1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guinea ya Ikweta yaacha kujenga ukuta mpakani mwa Cameroon

2 Julai 2020

Waziri wa Ulinzi wa Guinea ya Ikweta, Leandro Bakale amesema nchi hiyo imesimamisha kazi ya ujenzi wa ukuta kwenye mpaka wake na Cameroon.

https://p.dw.com/p/3eh1r
Bendera za Cameroon na Guinea ya Ikweta

Cameroon inaituhumu Guinea ya Ikweta kwa kujenga ukuta na kuingilia mpaka wake tangu Julai 2019, tuhuma ambazo serikali ya Malabo inakanusha. Mivutano kati ya nchi hizo mbili za Afrika ya Kati ilichochewa upya hivi karibuni wakati vyombo vya habari vya Cameroon viliripoti Juni kuwa Guinea ya Ikweta inajenga minara ya ulinzi kwenye mpaka huo. Pembezoni mwa mkutano wa kujadili mgogoro huo na mwenzake wa Guinea ya Ikweta katika mji mkuu wa Cameroon Yaounde Jumanne usiku, Waziri wa Ulinzi wa Cameroon Beti Assomo alizikaribisha ripoti za kusitishwa ujenzi huo. Waziri Bakale hakutaja suala la ukuta kwenye taarifa yake, lakini baadaye akawaambia wanahabari kuwa serikali yake inaihakikishia Cameroon fursa ya maridhiano.