1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Grossi aonya kuhusu hatari ya kukatika umeme Zaporizhzhia

9 Machi 2023

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Matumizi ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) Rafael Grossi, ameonya kuhusu hatari ya kukatika mara kwa mara kwa umeme katika kinu cha kuzalisha umeme cha Zaporizhzhia nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4OSzl
Österreich | IAEA Generaldirektor, Rafael Grossi
Picha: Heinz-Peter Bader/AP/picture alliance

Matamshi ya Grossi yanakuja  baada ya shambulio jipya la kombora kufanya kinu hicho kuendeshwa kwa jenereta za dizeli.

Grossi ameiambia bodi ya magavana wa shirika hilo kwamba umeme ni muhimu katika kuendesha pampu zinazosambaza maji kupoeza vinu na madimbwi yanayoshikilia mafuta ya nyuklia.
"Tunawezaje kuketi hapa katika chumba hiki asubuhi hii na kuruhusu hili litokee? Hili haliwezi kuendelea. Ninashangazwa na kuridhika, ndiyo, kuridhika. Tunafanya nini ili kuzuia hili lisitokee?" alisema Grossi.

Grossi amekuwa katika mazungumzo na Ukraine na Urusi kwa miezi kadhaa kujaribu kuweka eneo la ulinzi kuzunguka kinu hicho lakini mazungumzo hayo yanayonekana kukwama.