1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gordon Brown atangaza azma ya kutaka kumrithi Tony Blair

12 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2q

London:

Waziri wa fedha wa Uengereza Gordon Brown ametangaza rasmi azma ya kumrithi Tony Blair kama waziri mkuu na mwenyekiti wa chama cha Labour.Gordon Brown amesema amepania kubuni nafasi zaidi za kazi,kupambana na kitisho cha kigaidi na kitisho cha mabadiliko ya hali ya hewa na kujifunza kutokana na makosa yaliyofanyika katika vita vya Irak.Akihutubia mjini London,Gordon Brown amezungumzia umuhimu wa kurekebisha siasa za Uengereza kuelekea Irak.”Wakati umewadia wa kufuata mkondo mpya amesema bwana Gordon Brown na kusisitiza tunanukuu:”Tunabidi tuzingatie zaidi suluhu kati ya watu wa madhehebu tofauti na kuinua shughuli za kiuchumi ili wairak waweze kua na ushawishi mkubwa zaidi juu ya mustakbal wao.Mwisho wa kumnukuu waziri wa fedha wa Uengereza Gordon Brown.