Ghasia zaugubika uchaguzi Nigeria
10 Aprili 2011Matangazo
Bomu hilo liliripuka wakati maafisa wa tume ya uchaguzi walipokuwa wakihesabu kura kufuatia uchaguzi wa bunge hapo jana Jumamosi. Shambulio hilo linafuatia mengine kadhaa hapo Jumamosi na Ijumaa.
Makundi yanayohusika na masuala ya haki za binaadamu yanakadiria kuwa zaidi ya watu 80 wamekwishauawa kutokana na ghasia za kisiasa nchini Nigeria tokea mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka jana.
Baada ya kuahirishwa mara mbili kutokana na matatizo ya kiutawala, hatimaye uchaguzi huo ulifanyika hapo jana na utafuatiwa na ule wa urais wiki ijayo kabla ya kufanyika wa magavana wa majimbo yote 36 ya Nigeria tarehe 26 mwezi huu.
Mwandishi:Aboubakary Liongo/ZPR
Mhariri:Grace Kabogo