1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gharama za kuhifadhi wakimbizi Ujerumani

Abdu Mtullya25 Agosti 2016

Je, mpango wa kuwahudumia wakimbizi unaigharimu Ujerumani kiasi gani? Anaetaka kupiga hesabu atahitaji takwimu za uhakika. Hata hivyo mwandishi wetu Andreas Becker anasema ni vigumu takwimu za uhakika kupatikana.

https://p.dw.com/p/1JpTF
Deutschland Fingerabdruck Flüchtlinge
Picha: picture alliance/dpa/P. Endig

Takwimu hizo hazijawahi kuwa za uhakika hata mara moja. Kati ya mwanzoni mwa mwezi wa Sepetemba mwaka uliopita hadi mwishoni mwa mwezi ya juni mwaka huu, idadi iliyotolewa ilikuwa 900,623.

Lakini hesabu hiyo haiwezi kuaminika. Sababu ni kwamba wakimbizi wanaorodheshwa kwa siri, bila ya majina na bila ya namba za pasipoti zao.

Na msemaji wa Idara ya Wahamiaji na Wakimbizi, ameeleza kwamba pia inawezekana kwamba makosa yalifanyika katika mchakato wa kuwaandikisha wakimbizi.

"Kwa bahati mbaya, haiwezekani kusema ni wakimbizi wangapi walioandikishwa bado wapo nchini Ujerumani kwa sababu hakuna takwimu juu ya kila mtu binafsi," amesema msemaji wa Idara ya Wahamiaji na Wakimbizi.

Hatahivyo, msemaji huyo ameeleza kwamba ni jambo la uhakika kuwa idadi ya wakimbizi imepungua hivi karibuni.

Kwa mujibu wa takwimu, watu 16,000 waliingia Ujerumani mnamo mwezi wa Juni na katika mwezi wa Januari wakimbizi 91,000 waliandikishwa.

Lakini katika upande mwingine idadi ya watu walioomba hifadhi ya ukimbizi imeongezeka na mzigo umekuwa mkubwa kwa maafisa wanaowashughulikia watu hao. Kwa mujibu wa taarifa ya idara ya Ujerumani inayoshughulikia wahamiaji na wakimbizi maombi ya kwanza ya hifadhi ya ukimbizi mnamo mwaka uliopita yalifikia 441,899.

Na hadi kufikia mwishoni mwa mwezi wa Julai mnamo mwaka huu watu 468,762 walitoa maombi ya kupewa hifadhi ya ukimbizi nchini Ujerumani. Hata hivyo haijulikanai ni wangapi wataendelea kuishi nchini.

Katika mwaka uliopita maombi yaliyokubaliwa yalifikia asilimia 50 na mnamo mwaka huu ni zaidi ya asilimia 60.

Deutschland Erstaufnahmeeinrichtung für Flüchtlinge in Zirndorf bei Nürnberg
Jengo la Idara ya Wahamiaji na Wakimbizi mjini NürnbergPicha: Getty Images/J. Koch

Gharama au uwekezaji

Wakimbizi wanahitaji huduma za malazi, chakula na pia wanahitaji mafunzo.

Taasisi karibu zote zinakisia kwamba kila mkimbizi anaigharimu serikali ya Ujerumani kiasi cha Euro 12,000 hadi 20,000 kwa mwaka.

Kwa ujumla serikali ya Ujerumani inahitaji kiasi cha Euro, Bilioni 99 kwa mwaka kwa ajili ya kulipia gharama za wakimbizi.

Maoni yanatafutiana iwapo fedha hizo zinazotumika ni hasara au vitega uchumi.

Na ukweli ni kwamba fedha hizo zinarejea serikalini .Idara ya wakimbizi na wahamiaji imeongeza idadi ya wafanyakazi kutoka 3000 hadi 6000 mnamo kipindi cha nusu mwaka.

Mafunzo kwa wahamiaji

Pamoja na hayo serikali za majimbo zimeongeza nafasi 15, 813 za mafunzo ya kazi kwa ajili ya wakimbizi.

Walimu 25,000 watahitajika mashuleni na kwenye sehemu za mafunzo ya kazi.

Walezi wa watoto wapatao 14,000 pia watahitajika.

Gharama hizo zinazoonekana kuwa kubwa ni vitega uchumi vya siku za usoni. Ikiwa mchakato wa kuwaingiza wahamiaji katika jamii utaenda vizuri, serikali itaingiza mapato ya Euro Bilioni 20 katika kipindi cha miaka michache.

Lakini swali la kuuliza ni je wakimbizi wangapi watafanikiwa kupata ajira baada ya mafunzo?

Mwandishi: Becker Andreas

Mfasiri: Mtullya Abdu

Mhariri: Gakuba Daniel