MichezoUturuki
Ghana yamuaga Atsu aliyefariki kwenye tetemeko
17 Machi 2023Matangazo
Waombolezaji nchini humo walionekana kupanga mstari ili kumuaga mwanasoka huyo, Atsu ambaye jeneza lake lilikuwa limefungwa bendera ya taifa la Ghana. Atsu ambaye alikuwa na umri wa miaka 31 aliripotiwa kutojulikana aliko baada ya tetemeko la ardhi la Februari 6 kufuatia kuporomoka kwa jengo alimokuwa anaishi katika mji wa Hatay. Mwili wake ulipatikana kwenye vifusi na kusafirishwa hadi nchini Ghana.